Burudani

Ben Pol adai mapokezi ya wimbo ‘Phone’ yamemfanya ajipange upya kwenye video ya wimbo huo

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amesema mapokezi mazuri ya wimbo ‘Phone’ aliomshirikisha Mr. EAZI yamemfanya awekeze nguvu nyingi kwenye video ya wimbo huo.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo umekuwa mkubwa kwa muda mfupi tofauti na alivyotarajia.

“Kusema kweli namshukuru Mungu wimbo umekuwa mkubwa sana tofauti na nilivyotarajia, hata uwekezaji wa video nimelazimika kuwekeza zaidi kwa sababu nimegundua watu wanatarajia mambo makubwa. Kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna mazuri yanakuja kutoka kwenye video yake,” alisema Ben Pol.

Aliongeza, “Video naweza kusema ni kama tayari nusu, kwa sababu parts za Mr EAZI akiwa na mimi tayari pamoja na parts zake. Kilichobakia ni mimi kushoot sehemu zangu pamoja na story ya video na Mungu akisaidia ikakamilika mapema basi itatoka,”

Muimbaji huyo ni mmoka kati ya wasanii ambao ni zao la THT ambaye bado anafanya vizuri katika muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents