Michezo

Benitez: Kwangu Ilikuwa heshima kubwa kufanya kazi Real Madrid

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Real Madrid, Rafael Benitez amesema ilikuwa ‘heshima kubwa’ kuwa mkufunzi mkuu wa Real Madrid, siku moja baada yake kufutwa kazi klabu hiyo ya La Liga.

promo256550015

“Kama Mwanamadrid kutoka Madrid, anayeelewa utamaduni na maadili ya klabu hii, imekuwa heshima kubwa kufanyia kazi rangi hizi za klabu hii,” amesema kupitia taaifa.

Ameongeza: “Ningependa kushukuru kila mmoja ambaye tangu siku ya kwanza aliniunga mkono na kufanya kazi yangu kuwa rahisi.’

Raia huyo wa Mhispania Benitez, mwenye miaka 55, aliachishwa majukumu yake baada ya mkutano wa bodi ya klabu hiyo siku ya Jumatatu.

Nafasi yake alipewa mkufunzi mkuu wa timu B, mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane. Benitez alipoteza mechi tatu kati ya michezo 25 na kuwaongoza Real kufika hatua ya 16 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents