Habari

Benki ya NMB yawataka wakulima kuchukua mikopo ya pembejeo

Wakulima wa mkoa wa Katavi wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na taasisi za kifedha katika
kuchukua mikopo ya pembejeo ili kuinua kuwawezesha kufanya kilimo biashara na kukuza pato lao.

Washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya NMB.

Rai hiyo imetolewa na meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mpanda – Alex Massawe wakaati akifungua
mkutano maalum na wakulima na wafanyabishara wa mkoa huo.

Massawe amesema Benki ya NMB imekuwa ikikutana na wakulima wa maeneo tofauti kwa lengo la
kutoa elimu ya kilimo biashara ambayo itamsaidia mkulima kuleta tija katika kilimo.

Akizungumzia mikopo hiyo ya pembejeo, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kilimo Biashara Wogofya
Mfalamagoha amesema NMB inatoa mikopo ya pembejeo za aina tofauti kwa wakulima ambapo rejesho
lake ni mara moja tu kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu.

Aidha Mwakilishi kutoka NMB foundation – Rogers Shipela amethibitisha kuwa taasisi hiyo itaendelea
kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima

“Taasisi ya NMB foundation imeundwa kwa lengo la kutoa mafunzo ya ujasiriamali ambapo mkulima
ataweza kuuza mazao yake kwa bei itakayomnufaisha pamoja na hilo tunatoa elimu ya masoko ambayo
inatolewa ili mkulima aweze kuuza mazao yake kwa ufanisi “alisema

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents