Burudani

Besta akanusha kumpoteza Marlaw kwenye muziki

Msanii wa muziki, Besta ambaye pia ni mke wa Marlaw, amekanusha kumpoteza mume wake kwenye muziki.

marlawnabesta

Akizungumza leo kwenye U Heard ya Cloud FM, Besta alisema hawezi kumkataza Marlaw kufanya muziki.

“Kwanini nimkataze wakati na mimi nafanya muziki?” alihoji.

“Kwa sababu kama ningemkataza na mimi angenikataza kufanya muziki. Kila mtu anajipanga sio kukurupuka, sio kwa sababu tumeingia kwenye ndoa tuonyeshe ndoa yangu inafanya muziki ni kujipanga tu kazi yako ikiwa tayari tunatoa,” alisisitiza.

“Mtamsikia ana nyimbo nzuri sana, kila mtu ana vitu vyake binafsi, anafanya sio muziki peke yake na pia nashauri wasanii wengine wasitegemee muziki peke yake kwa sababu muziki huwa ni wa msimu. Kipindi ambacho hufanyi muziki utakuwa unafanya kitu gani kingine?”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents