Michezo

Bruno Fernandes yupo tayari kumalizana na United

Kiungo wa kati wa Manchester United Mreno Bruno Fernandes, 26,yuko tayari kumalizana na Mashetani hao wekundu kwa kusaini mkataba mpya ambao utaongeza mshahara wake mara dufu na kuweza kupata malipo ya takriban pauni 200,000 kwa wiki. (Sun)

Kiungo wa kati wa Manchester United Mreno Bruno Fernandes

Mlinzi wa Misri Ahmed Elmohamady, 33, ataondoka Aston Villa kwa mkataba usio na malipo msimu huu huku klabu hiyo ikiwa haina mipango ya kumpatia mkataba mpya. (Football Insider)Kalidou Koulibaly

Napoli wamepunguza kiwango cha pesa walizokuwa wanadai kwa ajili ya kumuuza Kalidou Koulibaly hadi kufikia kiwango cha euro milioni 45 (£38.7m), huku Bayern Munich wakiaminiwa kuwa mbele ya Liverpool na Manchester United katika mbio za kusaini mkataba na mlinzi huyo kutoka Senegal mwenye umri wa miaka 21. (Il Mattino – in Italian)

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate

Arsenal ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazoangalia uwezekano wa kumhamisha mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate mweye umri wa miaka 21. (Standard).

Konate ni mmoja kati ya wachezaji sita ambao Gunners wanashugulika kuwapata, huku klabu hiyo pia ikiwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Ufarnsa Alexandre Lacazette, 29, kwa bei inayofaa. (Football.London)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents