Habari

CHADEMA yapata pigo, Yakimbiwa na mjumbe wa bodi ya wadhamini

Aliyewahi kugombea Ubunge wa Jimbo la Ilala kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2015, Muslim Hassanali leo Jumanne Januari 9, 2018  ametangaza kukihama cha hicho na kujiunga CCM.

Muslim Hassanali

Hatua hiyo ya Hassanali inakuja katika kipindi ambacho wanasiasa wengi  wa vyama vya upinzani wakiwemo Wabunge na Madiwani wamekuwa wakivihama vyama vyao na kukimbilia CCM.

Kiongozi huyo ambaye pia alikuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa CHADEMA,  amepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula akiwa na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar es salaam.

Nimeikosoa serikali vya kutosha sasa nimeona ni wakati wa kushirikiana nayo kutekeleza yale ambayo nimekuwa nikiyasema kwa maslahi ya Watanzania,“amesema Muslim Hassanali.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amesema Hassanali ameomba kwa muda mrefu hivyo wameona hakuna jinsi zaidi ya kumruhusu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents