Burudani

Chris Brown kwenye tuhuma nzito ya kumpiga mwanamke, anachunguzwa (+ Video)

Staa wa muziki wa RnB kutoka nchini Marekani Christopher Maurice Brown alimaarufu Chris Brown usiku wa kuamkia leo ameripotiwa kuchunguzwa baada ya mwanamke mmoja kudai kumshambuliwa nyumbani kwake  huko Los Angeles mwishoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa zinadai kuwa ulitokea mzozo kati ya Breezy na mwanamke huyo ambaye jina lake halijawekwa wazi ndipo akampiga kofi kali mpaka kusababisha weave yake kutoka inagwa hakupata majeraha kando ya weave anayedaiwa kutolewa.

Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa lakini mamlaka ilithibitisha kwamba polisi walifika nyumbani kwake kufuatia tukio hilo linalodaiwa baada ya kutajwa kama mtuhumiwa katika ripoti ya polisi.

Bofya hapa chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/tv/CQa2-7Ehk7t/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents