Burudani

Christian Bella asema anasubiri ofa kubwa ili aonyeshe uwezo wake wa kuigiza

Mkali wa masauti Christian Bella amesema siku akipewa nafasi ya kuigiza na waigizaji wakubwa ataonyesha uwezo wake wa kuigiza.
bella

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Bella amesema anasubiria ofa kubwa ili aonyeshe uwezo wake wa kuigiza.

“Mimi sishindwi kuigiza kwa kweli, na kama ikitokea nafasi anaweza kufanya hivyo, issue ni mkwanja. Kama kuna msanii anataka kuwa na mimi kwenye filamu yake aweke tu mkwanja mezani alafu nimwonyeshe maajabu,” alisema Bella.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Nishike’, amesema anaamini hakuna msanii ambaye anashindwa kuigiza kwa kuwa sanaa zote zinaendana endana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents