Technology

Samsung yaanza kufidia wateja walionunua vimeo, Galaxy Note 7

Jumatatu hii, Samsung ilianzisha mchakato wa kuwafidia wateja walionunua simu hatari za Galaxy Note 7. Kazi hiyo imeanza Uingereza na Ireland.

samsung-galaxy-note-7

Kampuni hiyo imedai kuwa imerekebisha tatizo la betri katika simu hizo, lililosababisha kulipuka na itaanza kuwapa wateja walionunua simu zingine. Uingereza ni nchi ya kwanza kuanza kupokea simu hizo mpya za Note 7.

Kwa wateja wa Marekani wataanza kupata simu zao, Jumatano, September 21. Samsung iliingiza Galaxy Note 7 mwishoni mwa August, wiki chache kabla ya kuzinduliwa kwa iPhone 7 ya Apple, mpinzani wake mkuu.

Baada ya simu hizo kuonekana na tatizo la kuchemka, iliziondoa simu hizo sokoni. Kampuni hiyo ilikuwa imetengeneza simu hizo milioni 2.5 na tayari milioni 1 zilikuwa zimenunuliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents