Burudani

Exclusive: Christian Bella kufanya remix ya wimbo wa Ommy Dimpoz, Me and You

Muimbaji mahiri nchini, Christian Bella anatarajia kuurudia wimbo wa Ommy Dimpoz, Me and You. Akiongea na Bongo5, Bella amesema amefikia hatua hiyo kutokana na kuguswa mno na uzuri wa hit single hiyo na ngoma ya tatu ya Ommy Dimpoz.

14675_234921633307169_991886231_n

Amesema mara kwa mara alipokuwa akikutana na Ommy alikuwa akimuimbia wimbo huo na hatimaye Ommy alimwambia afanye remix yake.

“Mwisho wa siku ikabidi aniambie ‘basi Bella mimi nakuruhusu iimbe hii nyimbo, mimi nataka upigi remix ya hii nyimbo’. Kama utani tu, nikaona ni good idea kwasababu wenzetu nao Ulaya wanafanyaga hivyo, kama mtu akipenda wimbo anaweza kwenda kwa mwenye huo wimbo akamwambia ‘mimi nataka nifanye remix. Lakini hiyo tulivyokaa Dimpoz mwenyewe ndio aliniambia mimi hivyo,” amesema.

Bella amesema remix yake kwa wimbo huo itakuwa na mahadhi ya R&B. Pia muimbaji huyo wa nyimbo kama Msaliti na Usilie aliomshirikisha Banana Zorro amesema atamshirikisha Ommy Dimpoz kwenye wimbo wake uitwao Nani Kama Mama.

Msikilize hapa akiongea na kuimba kipande cha wimbo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents