Burudani

Collabo ya Wizkid na Diamond haiepukiki

Diamond Platnumz amefanya collabo na kila msanii mkubwa wa Nigeria.

12132711_482048025296498_1976295501_n

Ameshafanya ngoma au kushiriki kwenye ngoma na P-Square, Davido, D’Banj, Tiwa Savage, Iyanya, Waje, Kcee, Bracket, Flavour na wengine lakini ni msanii mmoja tu mkubwa hajakutana naye kwenye wimbo wowote – Wizkid.

Wawili hao walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye show ya Leaders Club jijini Dar es Salaam, na picha zinaonesha kuwa tayari zimeiva, licha ya ukweli kuwa huenda wamewahi kuwasiliana kabla ya hapo.

Baada tu ya show yao ya Leaders wawili hao hawakuwa wachoyo kwa mashabiki wao kuwaonesha kuwa mazungumzo ya kazi za baadaye yameanza.

12145462_495574617277488_101970387_n

Wikzid alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Nana na kuandika, “Big up to @diamondplatnumz for the love!! We link up soon!! #OneAfrica.”

Naye Diamond alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Ojuelegba na kuandika, “When they ask you, what was the name of the food you ate in Tanzania… tell them “Ubwabwa na Kuku” @wizkidayo.”

Wizkid atarejea tena December kwenye Fiesta na huenda kile mashabiki wamekililia kwa muda mrefu kati ya mastaa hawa kitakamilika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents