Burudani

Darassa kuja na mradi wa ‘Magic Muziki’

Rapper Darassa amesema ameamua kuanzisha kundi la muziki liitwalo ‘Magic Muziki’ litakalokuwa likiunganisha wasanii wachanga na ambao atakuwa akiwasaidia kimuziki.

11887103_131215600554931_1487815211_n

Darassa amesema ameamua kuanzisha kundi hilo ili aweze kuwasaidia wasanii hao kwa pamoja.

“Tayari kuna project kadhaa nimesharekodi, ngoma nimetunga mimi, nimewapeleka studio madogo na mpaka sasa kazi ipo safi. Hawa wasanii watakuwa wanaitwa Magic Muziki, ni kama kundi fulani. Kwahiyo watu wategemee baada ya kumaliza kazi zangu nadhani mwezi wa kumi na moja kazi zao zitaanza kusikika,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents