Burudani

Davido kutambulisha video 5 mpya ambazo hakuwahi kuzitoa Jumamosi hii kupitia MTV Base

Staa wa Nigeria, Davido ana video 5 kwenye maktaba yake ambazo hakuwahi kuzitoa, lakini amepanga kuzitambulisha kwa mashabiki wake Jumamosi hii (Oct.10).

Davido A

Wasanii huwa wana tabia ya kurekodi nyimbo nyingi ambazo baadae huja kuzichuja ili kupata zile kali zaidi za kutoa na zingine kuziweka kwenye album, lakini kuna zingine huwa zinaachwa kabisa endapo kukiwa na nyingine kali zaidi.

Davido anatarajia kuwaonesha mashabiki wake video 5 ambazo hakuwahi kuzitoa, lakini ni za nyimbo za album yake ya kwanza OBO Genesis’, kupitia MTV Base kwenye kipindi kilichopewa jina la ‘Davido Exposed’ siku ya Jumamosi October 10, 2015, siku ambayo pia ataachia album yake mpya ‘Baddest’.

Video hizo ni New Skul Tinz, Bless Me, Dollars in The Bank, Video na MaryJane.

Kipindi hicho kitaruka Jumamosi 3pm, na kurudiwa Jumapili 12pm, Jumatatu 2pm na Jumatano 7pm WAT.

Davido pia amesema ana mpango wa kushoot video mpya Tokyo, Japan ama Jamaica kwasababu hakuna msanii wa Nigeria aliyewahi kufanya video kwenye nchi hizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents