Burudani

Daxo Chali alikuwa ananitaka hadi anatumia nguvu – Haitham

Ishu ya msanii Haitham kutilimuliwa MJ Records na producer Daxo Chali imechukua sura mpya mara baada ya msanii huyo kudai kuwa Daxo alikuwa anamtaka kimapenzi.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Play Boy’ ameiambia FNL ya EATV kuwa amefanya kazi na Daxo kwa kipindi cha miaka mitano na kuna mambo mengi yaliyotokea ila hilo la kumtaka kimapenzi ni moja wapo ingawa kwake hakuwahi kufikiria na ni kitu ambacho hakitakaa kutokea.

“Off course mara nyingi, mara kibao yani tena sometime hadi kwa kutumia nguvu kwa sababu mimi nimekutana na Daxo miaka mitano, so nina vitu vingi hivi nilivyoongea ni vichache ingawa vya ndani zaidi siwezi kuviongea” amesema.

“Sometime mpo studio zile night mmerekodi mmechoka anaweza kuja na stori fulani wewe ukawa huzielewi halafu ukiangalia mtu mwenyewe anayekuambia hivyo vitu siyo type yako, yaani ni mtu ambaye huwezi kuwa na hisia naye hata ukimwangalia mara mbili mbili, mmmh!!! hapana” amesisitiza.

Haitham pamoja na msanii mwenzake Nini walitimuliwa MJ Records na Daxo Chali kwa kile kilichodaiwa kwenda kinyume na taratibu za label hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents