Habari

D’Banj atajwa ‘Best African Act, 2012’ kuwania MTV Europe Music Awards

MTV imemtangaza supastaa wa Nigeria D’banj kuwania kipengele cha ‘Best African Act of the 2012’ katika tuzo za MTV Europe Music kwa kupata kura nyingi zaidi kutoka kwa mashabiki wa Afrika.

D’Banj ambaye jina lake halisi ni Dapo Daniel Oyebanjo amewashinda wakenya Camp Mulla, mnaijeria mwenzake Wiz Kid, Sarkodie wa Ghana na Mi Casa wa Afrika Kusini.

Tuzo hizo zitaendeshwa na supermodel Heidi Klum na kufanyika nchini Ujerumani kwenye jiji la Frankfurt November 11.

Msanii huyo sasa atashindana na wanamuziki wa India, Alobo Naga & the Band na Ahmed Soultan wa mashariki ya kati kuwania kipengele kikubwa zaidi cha duniani ambapo MTV inaangalia muziki wote wa dunia.

Kuanzia October 30, mashabiki wataweza kuwapigia kura wasanii kutoka mabara tofauti kupitia www.mtvema.com.

Wawakilishi wa maeneo ya Africa/India/Middle East watatangazwa Jumanne ya October 30 pamoja na washindi kutoka maeneo ya Ulaya, Latin America, America Kaskazini na Asia Pacific.

Watajwa hawa wa maeneo hayo matano watashindania kura za kushinda tuzo ya “Worldwide Act” na mshindi atatangazwa kwenye show hiyo ya Frankfurt.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents