Habari

DC Jerry Murro afunguka sakata la kutoa gari la serikali kwa Lemutuz

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Murro amekanusha taarifa ambayo ameitoa Lemutuz kupitia mitandao ya kijamii kwamba alipewa gari la serikali kwaajili ya kutembelea.

Lemutuz akiwa mbele ya gari za viongozi

Mapema jana wadau mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii walimshambulia mwanamitandao huyo baada ya kupost picha na kudai kwamba alitumiwa gari la serikali kwaajili ya kupokewa wakati anaingia wilayani Arumeru.

“Wote tunamjua Lemutuz tambo zake huko kwenye mitandao ya kijamii, nisingeweza kubishana naye kuhusu alichokiandika kwenye ukurasa wake, ningekuwa namvunjia heshima yule ni kaka yetu, najua sheria siwezi kutoa gari ya serikali” alisema DC Jerry kupitia 360 ya Clouds TV

Aliongeza, “Niwaombe Watanzania isifike mahali mtu akaogopa kupiga picha kwenye magari ya kodi zao kwa kuwa akipiga picha italeta maana tofauti”


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents