Burudani

Diamond kwenye jarida la Billboard “Wasanii wa Marekani wajifunze kuitumia Youtube kutoka kwa Diamond”

Katika ahbari kubwa siku ya leo ambayo imeshika vichwa vya habari duniani kote ni hii iliyotolewa na jarida la @Billboard wakielezea na kuwashauri wasanii wa Kimagharibi namna ya kupata mafanikio kimataifa kwa kutumia mtandao wa @Youtube huku wakimtolea mfano msanii kutoka Tanzania @Diamondplatnumz

Kichwa cha habari katika makala hiyo kinasomeka hivi:-  “Wanamuziki wa Marekani wanaotaka kuwasha moto kupitia Youtube, Wanapaswa kujifunza mikakati hii kutoka kwa wasanii wa Kiafrika”
.
Amezungumza meneja wa ‘Youtube Music Trends’ Kevin Meenan, ambaye anasimamia ukusanyaji na uchambuzi wa data za chati za Muziki za YouTube “Wasanii wa Magharibi wanaweza kujifunza kutoka kwa kile wanachokifanya wasanii wa Kiafrika haswa wale ambao wamefanikiwa kimataifa,”
Ameelezea kuwa alivutiwa sana na mbinu pamoja na ubunifu ambao anautumia msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz kwenye chaneli yake ya YouTube na sehemu moja tu ya mkakati wa ujasiriamali ambao unajumuisha kituo cha redio ya FM pamoja na TV na usimamizi wa kampuni ya WASAFI.Kevin Meenan amesema Ukubwa wa Diamond kwenye Youtube ni wa kustaajabisha akiwa na Subscribers Millioni 3.6 na zaidi ya jumla ya views Millioni 980 huku 80% ya watamazaji wakiwa wanatokea nje ya Tanzania kutoka Mei 1, 2019 hadi Mei 1, 2020Aliongeza kuwa, kimataifa Diamond alitazamwa zaidi na watu wa Nchini Kenya ikifuatiwa na Tanzania na Marekani.
.
Billboard wameeleza kuwa Msimamizi huyo wa Youtube Trending alishangazwa kukuta Diamond ameweka zaidi ya video 600 kwenye mtandao wa Youtube “Kwa kweli ilibidi nichunguze mara tatu ili kuhakikisha kuwa ilikuwa sawa,”
Wamesifia kuwa Diamond anaweza kuweka hadi video 20 akitangaza Official video moja tu huku wakitolea mfano wa wimbo wa Jeje ambapo ukiachana na Official video, kuna dance video, cartoon video, lyrics video pamoja na official audio.

Kwenye Makala hiyo Billboard wameelezea kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa wasanii wengi ambao wamefanikiwa kufikisha subscribers zaidi ya Million 1 basi huwa wanatazamwa zaidi na watu wa nje ya nchi zao.

https://www.youtube.com/watch?v=DvMMZX92gaw
Wamesema Kevin Meenan amewahi kufanya uchunguzi wa kuangalia chart ya Top 100 ya Tanzania na Nigeria na kulikuwa kuna nyimbo 8 ambazo zinatrend pote, huku Tanzania na Marekani zikiwa na nyimbo 4 ambazo zina Trend pote.
Matokeo mengine ambayo timu za Muziki za YouTube na Tamaduni na mwenendo wa YouTube ilizigundua ni kwamba
• “idadi kubwa” ya maoni ya YouTube kwa wasanii wa kiafrika ambao wana Subsriber zaidi ya  milioni 1 – kati yao Wizkid, Yemi Alade, Davido, Burna Boy na Naira Marley – “hutoka nje ya nchi ambayo wametoka,” anasema Meenan, akimtaja Burna Boy na Davido kama mifano. “Asilimia 95 ya maoni Youtube  yanakuja kutoka nje ya Nigeria.” Katika visa vyote viwili, Iliongoza kwa maoni zai Kwa Burna Boy,huku  Ufaransa na Uingereza ziliweka za pili na tatu na kwa Davido ikiwa hivyo hivyo.
https://www.youtube.com/watch?v=DvMMZX92gaw
Chanzo:-
https://www.billboard.com/articles/business/9393686/how-to-go-global-on-youtube-watch-and-learn-from-africas-top-music-stars
https://www.youtube.com/watch?v=DvMMZX92gaw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents