Burudani

Diddy, DJ Khaled kuibuka katika TV Show

Diddy na DJ Khaled wapo katika mazungumzo makubwa na Fox kwa ajili ya tv show mpya ya kusaka vipaji, “The Four,” ambayo itakuwa ya tofauti na nyinginezo za hapo awali.

Diddy na DJ Khaled

Vyanzo vya habari vinavyoaminika vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa hakuna hata mmoja aliyesaini hadi sasa lakini mazungumzo yamefikia katika hatua nzuri.

Inaelezwa kuwa kutakuwa na majaji wanne ambapo Diddy atakuwa kiongozi, huku DJ Khaled ni mtayarishaji, pia kutakuwa na mwandishi wa nyimbo, na jajiĀ  wa nne atakuwa upande wa utumbuizaji, pia katika nafasi hizo kutakua na mwanamke angalau mmoja.

Kipande kikuu cha show kitakuwa pop ila msisitizo zaidi ni katika hip hop. Itakuwa vita inayoendelea katika mtindo wa kuchanana mbele ya watazamaji na hatimaye mshindi atapatikana kutoka kwa majiji wote. Hata hivyo hakuna taarifa show itakuwa wakati gani lakini inaeezwa kuwa na ladhaa ya tofauti na yenye kuvutia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents