Burudani

Diddy na Cassie warudiana baada ya kuachana kwa ugomvi mzito

Baada ya kumwagana kwa ugomvi mzito siku chache zilizopita, Cassie amebadili moyo wake na kurudi kwa Diddy, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.

cassie-diddy

Chanzo cha ugomvi wao ilidaiwa ulitokana na mabishano makali kati yao wakiwa kwenye gari Jumatano mchana ya wiki iliyopita baada ya Cassie kumwambia Diddy kuwa anataka waachane, kitendo kilichomkasirisha Diddy kiasi cha kushika simu na mkewe na kuanza kuikagua na baadaye akaondoka nayo lakini baada ya muda alimrudishia.

Ugomvi huo uliwahusisha mpaka polisi wa Beverly Hills waliofika nyumbani kwa Cassie walioitwa na mama yake lakini hata hivyo aliwaeleza kuwa ameipata simu yake na wakaondoka japo waliandika ripoti ya tukio hilo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Diddy amemtumia ujumbe wa siku ya kuzaliwa mpenzi wake huyo, ameandika, “HAPPY BIRTHDAY BABY! @cassie I LOVE YOU ALWAYS. GOD BLESS YOU????????❤️❤️❤️????????????????.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents