Burudani

Davido atangaza ujio wa albamu yake mpya Septemba mwaka huu

Davido amethibitisha kuachia albamu yake mpya mwezi Septemba mwaka huu.

Davido

Albamu hiyo imepewa jina la ‘Son of Mercy’ na inatarajiwa kuwa na nyimbo zisizopungua 10. Kupitia mtandao wa Instagram, Davido ameandika, “SEPTEMBER WE BEGIN THE JOURNEY TO THE ‘SON OF MERCY’ DOUBLE E.P !!!.”

Mpaka sasa Davido ameshaachia albamu nne ikiwemo ‘Omo Baba Olow’, ‘The Baddest’, ‘Gobe’ na ‘Best Of Davido’. Tangu mwezi Januari mwaka huu msanii huyo alipo saini dili na kampuni ya Sony Music ameonekana kuwa kimya bila ya kuachia wimbo wowote lakini amekuwa akionekana na mastaa kadhaa kama Trey Songz, Dj Snake, Usher Raymond na wengine wengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents