Burudani

Dogo Janja ana sababu za kwanini ngoma za Hip Hop hazifanyi vizuri

Dogo Janja ana sababu kadhaa za kwanini ngoma nyingi za wasanii wa Hip Hop zinashindwa kufanya vizuri.

Dogo Janja

Rapper huyo aliyekaa kimya kwa muda wa mwaka mzima bila kutoa wimbo, ameiambia Bongo5 kuwa tatizo kubwa kwa wasanii wa Hip Hop ni kutotilia maanani suala la video nzuri.

“Kwanza muziki umebadilika na mfumo mzima wa muziki umebadilika,” anasema rapper huyo wa Tip Top Connection.

“Sasa hivi watu wengi wanaamini kwamba video kali inaweza kumfikisha msanii mbali. Sasa unakuta wasanii wengi wa Hip Hop wanaweza kutoa audio halafu video kimya. Sasa hivi tunatakiwa kuboresha sanaa zetu kwenye video, upande wa nyimbo zisiwe ngumu sana ziwe za kawaida, yaAni ziwe ki-commercial. Sasa hivi usipotoa ngoma ngumu ukidhani watu wataumiza kichwa kuusikiliza umeumia. Mashabiki wengi wakiona wimbo hawauelewi wanaacha nao,” amesisitiza.

“Kwahiyo sasa hivi ukiwa na audio lazima uwe na video kali. Sasa hivi kinachowaangusha rapper wengi ni video. Unajua sometimes mtu anaogopa kuwekeza katika video, wanafanya ngoma kali sana wana flow vizuri lakini tatizo linakuja kwenye video, lakini wakikomaa tu wanatoboa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents