Michezo

Dylan Kerr asema timu yake itacheza bila hofu ya Rooney

Kocha wa timu ya Gor Mahia, Dylan Kerr amesema ugeni wake ndani ya timu hiyo hauwezi kumfanya ashindwe kuisaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya Everton ya nchini Uingereza.

Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr (katikati) akiwa na kapteni wa timu hiyo, Musa Mohammed

Muingereza huyo ana wiki moja toka atangazwe na bodi ya timu hiyo wiki moja iliyopita akichukua mikoba Jose Marcelo ‘Ze Maria’ ambaye aliisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa wa Sportpesa Super Cup.

Akiongea na waandishi wa habari jioni hii ndani ya Uwanja wa Taifa, Kocha huyo amesema ugeni wake ndani ya kikosi hicho hauwezi kuikwamisha timu hiyo kushinda mchezo huyo.

“Gor Mahia tumejiandaa vizuri sana kwaajili ya Everton hapo kesho, mazoezi yamendelea vizuri. Rooney ni mchezaji mzuri lakini sisi pia tumejipanga kukabiliano nao na pia kushinda mechi,” alisema Kerr.

Kwa upande wa kapteni wa timu hiyo, Musa Mohammed amesema ugeni wa kocha wao hauwezi kuwa changamoto ya kuwafanya washindwe kupata matokeo.

“Timu mzima tumejipanga vizuri sana na mungu akisaidia tutashinda kwa sababu Everton ni timu ambayo inafungika. Suala kocha mpya sio tatizo kwetu kwa sababu timu kama timu ni ile ile na yeye amekuja kutupatia mbinu mpya ambazo zitaidaidia timu kuibuka na ushindi,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents