Habari

Eid Alhaj: Relief Organisation yagawa nyama kwa wasiojiweza (Picha)

Taasisi ya African Relief Organisation kupitia shirika la Rahma International imeanza kugawa nyama katika misikiti, vituo vya watu wenye mahitaji maalum nchini ili waweze kusherehekea sikukuu ya Eid Alhaji.

Naibu Mkurugenzi wa African Relief Organizations, Ibrahim Yussuph akindaa nyama kwaajili ya kutoa msaada kwa watu wasio na uwezo.

Mgao huo umeanza katika jiji la Dar es Salaam, ambapo taasisi hiyo imeanza kuchinja ng’ombe 40 kondoo 100 na mbuzi 100.

Akizungumza wakati wa sikukuu ya Eid Alhaj Dar es salaam Ijumaa hii, Naibu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Ibrahim Yusuph nia ni kutekeleza maelekezo kuhusu katika kusherehekea sikukuu hiyo ambapo ni muhumu kusaidia wale ambao hawakujaaliwa kuweza kuchinja.

“Eid Elhaji ni sikukuu ambayo tunasherehekea baada ya kukamilisha ibada ya Hija.Mara nyingi tunamalizaia kwa kuchinja wanyama, lakini tunaelekezwa kusaidia wale ambao hawakujaliwa kipato cha kuwawezesha kuchinja,”alisema Yusuf.

Alisema taasisi yake itaendelea kugawa nyama kadri itakavyoweza kwenye misikiti, vituo vya watu wenye mahitaji maalum, yatima na ambao hawakujaaliwa kipato.

Afisa habari wa taasisi hiyo, Jamal Suleiman alisema dini ya kiislamu inaagiza kusaidiana ambapo mgao wa nyama utahusisha mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Lindi, Mtwara, Singida na Kilimanjaro.

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally (katikati) akisalimiana na baadhi ya masheikh katika ibada ya Eid al-Adha iliyofanyika katika msikiti wa Masjid Taqwa Ilala Bungoni jijini Dar es salaam.


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Alhad Mussa Salum akisalimiana na baadhi ya masheikh.


Nyama ya ng’ombe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents