Burudani

El Saadat Nyoshi kwenda Ulaya kujifunza utayarishaji wa muziki

Kiongozi wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat amesema anatarajia kwenda Ulaya kujifunza utayarishaji wa muziki ili akiachana na kazi ya muziki wa bendi afanye kazi hiyo.

nyoshi-el-saadat

Akizungumza na gazeti la Mtanzania hivi karibuni El Saadat amesema malengo yake ni kujifunza maswala mbalimbali yafusuyo studio pamoja na kujiwekea malengo hayo kwa kuwa hana tena moyo wa kufanya kazi kwenye bendi nyingine nchini. “Sifikirii kwenda kufanya kazi katika bendi yoyote zaidi ya iliyopo sasa,siku nikiamua kuachana nayo naelekea Ulaya kujifunza mambo ya studio,” alisema.

Saadat amesema hakuna bendi ambayo imemvutia kufanya nayo kazi zaidi ya FM Academia na bendi nyingine zilizobaki ni ubabaishaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents