Burudani

Ellen Johnson ashinda Tuzo ya Mo Ibrahim

Rais wa Mstaafu wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim kwa Uongozi wa Afrika. Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao wameonekana kuwa na utawala mzuri.

Kamati ya Utendaji ya tuzo ya Mo Ibrahim imesema Ellen Johnson Sirleaf ameonesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.

Kutokana na kushinda tuzo hiyo Ellen Johnson Sirleaf atapata dola za Kimarekani milioni tano zitakazogawanywa kwa miaka kumi, na dola laki mbili kwa maisha yake yote.

Kamati ya utendaji ya Mo Ibrahimu imesema kwamba inafahamu mapungufu yake lakini imeamua kwamba anastahili kupata tuzo hiyo.

Mjasiriamali Mwingereza mwenye asili ya Sudan Mo Ibrahim alianzisha tuzo hiyo mwaka 2007 kwa ajili ya kuwatunukia viongozi walionesha kazi nzuri wakati wa kipindi cha uongozi wao ndani ya bara la Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents