Exclusive Interview: Dayna akizungumzia sakata la beat ya wimbo wake kutumiwa na Diamond kwenye Number 1 (Audio)

Apparently wimbo mpya wa Diamond, Number 1 ambao video yake ilifanyika nchini Afrika Kusini na kuzinduliwa wiki iliyopita, umetumia beat ya wimbo wa Dayna Nyange uliokuwa umerekodiwa tayari na alipanga amshirikishe Diamond.

IMG_5897
Dayna Nyange

Dayna aliyewahi kuhit na wimbo Nivute Kwako, ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo aliurekodi muda mrefu na alikuwa akimsubiri tu Diamond aingize sehemu yake lakini mara nyingi haikuwa rahisi kutokana na ubusy wake na tayari alikuwa amemsikiizisha demo yake.

“Tulisikiliza ule wimbo kwenye gari yake, akasikiliza kama mara tatu hivi akaniambia ‘kazi ni nzuri tunaweza tukafanya kitu,” anasema Dayna.

“Ni track ambayo nilikuwa naitegemea na nilikuwa naiamini,”aliongeza.”Ukimuangalia Diamond ni mtu ambaye mimi simfikii kisanaa, ni mtu ambaye tayari kafika mbali, kwahiyo nilijua hata nikikaa naye kwenye ile kazi, ni kazi ambayo na mimi ingeweza kunisogeza sehemu fulani.”

Sikiliza wimbo wa Dayna hapo chini.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/108788537″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Anasema baada ya kumsikilizisha wimbo huo, wakapanga Diamond akafanya kipande chake lakini ratiba zao zilikuwa zinapishana. Dayna anasema baada ya muda kupita alikuja kupigiwa simu na mtu aliyedai ameusikia wimbo wa Diamond uliotumia beat yake lakini hakuamini.

“Kwa mazingira yale tuliyokuwa tumeanza na ile kazi mwanzoni mpaka kusikia eti nakuja kuambiwa hivyo mimi nilikataa sana.”

Baada ya kushindwa kuamini, mtu huyo alimtumia wimbo huo wa Diamond kipindi ambacho ulikuwa haujatoka na kuamini kweli beat yake imetumika. Dayna anasema anakumbuka Diamond hajawahi kwenda kwenye studio ya Sheddy Clever, producer wa wimbo huo kitendo ambacho anasema kimetokea baada ya kuwa ameusikia wimbo wa Dayna na kuupenda na hivyo kumfuata producer huyo na kumshawishi beat aitumie yeye.

“Kwenda kwake kwa Sheddy, alikwenda kitofauti kwamba kwa lengo la kunizunguka mimi na kwenda kuitumia ile beat,” anasema Dayna.

“Baada ya kupata uhakika wa hicho kitu kiasi fulani kwanza kilinivunja moyo na kilinivunja nguvu ya kufanya kitu chochote,” anaelezea Dayna kuhusiana na jinsi alivyojisikia baada ya kuujua ukweli na hata hivyo anasema hakuweza kumpigia simu Diamond.

Sikiliza wimbo wa Diamond hapo chini.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/108788682″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

“Kwasababu kwa upande wangu mimi, nilijiuliza maswali kama nikimpigia simu Diamond namuuliza, ‘Diamond kwanini umetumia beat yangu’ wakati najua kweli ametumia beat yangu?” anahoji msanii huyo.

“Kwahiyo mimi sikuweza kumpigia simu tena Diamond na Sheddy kwasababu nilishawahi kumpigia simu akaniambia kwamba hakijafanyika kitu, kwahiyo nikajua kabisa hawa walishakaa, wakakubaliana ndo wakaamua kulifanya.

Diamond ni mtu ambaye nilikuwa namheshimu sana na nilikuwa namkubali sana kutoka moyoni mwangu japo kila mtu na mapungufu yake na nilimuamini sana kiasi kwamba hiki kitu alichonifanyia yaani kimenivunja moyo kweli, kimeniuza kweli.”

Amesema kwa sasa kuna ushauri aliopewa kuufanya ili kupata suluhisho la hicho kilichotokea na atatoa taarifa baadaye.

Wakati huo juhudi za kumpata producer wa wimbo huo, Sheddy Clever ili azungumzie upande wake zimegonga mwamba kwakuwa hapokei simu zetu na Diamond yupo nchini Kenya kikazi.

Related Articles

Back to top button