Burudani

Exclusive: Izzo B azungumza baada ya video ya ‘Love Me’ kupitishwa Channel O

“Hakika Mungu mkubwa Channel 0 wameipitisha video ya ” Love Me ” bado kuanza kuruka tu shukrani za dhati kwa @jokateM na watu wangu wote,” ametweet Izzo Bizness na sisi kuamua kumtafuta kwa simu kuongeza naye zaidi.

http://www.youtube.com/watch?v=lqdfYuP_0LM

“Imepita tu katika hatua za kwanza kwamba inastahili kuchezwa ,” amesema Izzo na kuongeza kuwa bado haijanza kuonekana kwenye mzunguko wa video zinazochezwa kwenye kituo hicho cha runinga cha nchini Afrika Kusini.

Love Me inakuwa video ya kwanza katika career ya Izzo ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Simwinga kupitishwa kwenye kituo hicho.

“Video nyingi tulikuwa tunatuma sijui tatizo lilikuwa ni nini labda zilikuwa hazifikii vigezo au labda kuna connection fulani tulikuwa tunazikosa.”

Hata hivyo Izzo amesema mapokezi ya video ya Love Me yamekuwa makubwa kuliko video zote alizowahi kuzifanya awali.

“Video imekuwa na mapokezi makubwa sana, kitu ambacho kimenipa faraja sana,” ameongeza Izzo.

Akimzungumzia director wa video hiyo, Nick Dizzo, Izzo amesema ni muongozaji mwenye uwezo mkubwa kama msanii ukijiandaa vizuri kufanya naye video japo watu wanamchukulia poa.

“Kuna watu wengi wanamchukuliaga rahisi lakini kama unajipanga na unampa moyo wako kweli na yeye anagundua hilo lazima mfanye kazi nzuri.”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents