Exclusive: Shaa azungumza namna ‘Baba Kodi’ ilivyoleak, video ya Lava Lava na mtazamo wake kuhusu digitali

Hivi karibuni Bongo5 ilipiga story na Saraha Kaisi aka Shaa kuhusu masuala mbalimbali ikiwa pamoja na jinsi wimbo wake ‘Baba Kodi’ ulivyoleak, video ya Lava Lava na namna mfumo wa digitali ulivyomuathiri kazi zake.

shaaKuhusu kuleak kwa ‘Baba Kodi’

Ile ngoma tuliimaliza like last year kwahiyo tukawa tunayo tunaisikiliza here and there katika uamuzi wa wimbo gani wa kwanza kutoa ikiwemo it was on the list lakini tukaamua tuanze na promise tukasema ile ngoma ya “baba kodi itakuja kutoka karibu na mwisho wa mwaka ambapo ndio watu wengi wanakuwaga na issue za kodi, tukakubalianah ivyo sawasawa naona Babu Tale aliupenda sana akasema ‘subiri niwasogezee wadau kadhaa wausikie halafu tusikie their opinion’ kwasababu yeye alikuwa anataka uwahi kutoka, alitaka utoke mwanzo wa mwaka.Kwahiyo akausogeza toka last year December, tulivyoona nothing happened nini ,sisi tukaendelea na mipango yetu tukatoa Promise nini wimbo umetoka.

Next thing I know on twitter you guys ndio mnanishtua. So when I read the tweet kuhusu Baba Kodi, nikasema hiii, hawa wameusikia wapi? So nikampigia Master pale nikamuuliza did you know Baba kodi is coming out? Akaniambia mimi mwenyewe nimeshtuliwa like a few minute ago. Nikamwambia can you please investigate what happened, how did the song came out. Kwababu huu ni mwaka wangu wa nne in the game sijawahi kulikisha kuleak hata wimbo mmoja and I have done over twenty songs. So I wanted to know what is the source ili isinitokee again. So tukaulizia hapa na pale ndo Jay akaniambia kwakweli the first mtu niliyefikiria alikuwa ni Manecky kwasababu yeye ndiyo kauproduce yeye ndiyo yupo pale studio.

Lakini Manecky according to him ni kwamba alinipa mimi na Babu Tale, so Jay akasema ‘mimi sijampa mtu yoyote the only person here ni Babu Tale’. So akampigia Babu Tale akamuuliza umesikia wimbo umetoka? Akasema ‘ndiyo ndiyo umeona mkali, umeupenda?’

Jay akamwambia sawa tunashukuru wimbo umependwa lakini umetokaje tokaje? how did people get it? Ndo Babu Tale akasema, ‘unajua muda ule kuna watu wawili watatu niliwasogezea ili wausikie’ so it’s possible kwamba ilikuwa hivyo, halafu mmoja aliusogeza via whatsup na mmoja BBM, kwahiyo akasema it’s possible that, you it spread out like that, ndiyo tukajua kwamba since Babu Tale mwenyewe ndiyo aliadmit kwamba aliwapa few people itakuwa imetoka from there. Kwahiyo it’s from Babu Tale trusting watu ambao siyo ndio maana wimbo umetoka.

Nashukuru kwamba yaani watu wameupokea vizuri even though my initial plan ilikuwa nikuutoa the end of the year na ilikuwa tuutoe na video kwasababu ni wimbo ambao idea ni ya Adam Juma. Adam ndio alinitafuta mimi akaniambia, ‘nina bonge la idea for you’ nikamwambia what? akaniambia I am thinking of a song called Baba Kodi halafu baba kodi anakusumbua, baba kodi this this’. Kwahiyo Adam hada vision ,Adam akaundika half way akaniambia mimi nitaandika the chorus wewe andika the verses. Ulikuwa ni ushirikiano between me and Adam, kwahiyo hata Adam alivyopata hizo news akatupigia akasema ‘what happened, I thought you know we are working together’.

Kwahiyo mimi nilimind kihivyo kwamba vilevile imenicost kidogo like a problem kidogo with Adam kwamba asije akaona nimeenda behind his back. Kwahiyo nikamwelimisha tu na Adam na akasema, ‘hata hivyo the song it’s tight anyway let’s just do a video’. So you know nashukuru kwamba hajaichukulia vibaya one, two nashukuru kwamba huu wimbo ulikuwa umeshamalizika kuliko wimbo ungetoka haujamixiwa au sijamaliza the vocals sijui hata mashabiki wangu wangenielewaje, kwasababu I always make sure kwamba, whatever I deliver is a hundred percent so ingetoka half way sijui mngenisomaje? Kwahiyo nashukuru kwamba it came out that way.

Kuhusu video ya Lava Lava

Kwa bongo hapa ilikuwa tuanze na Promise halafu nilikuwa nitoe Lava Lava kwaajili ya soko langu la nje la Africa kwasababu sijatoa wimbo mwaka jana at all so nikaona mwaka huu nikaona siyo mbaya nikitoa nice song a nice video ambayo hata Dar hapa pia nitaitoa kwa sababu ni nyumbani lakini the focus ni nje, East Africa ,West Africa, South Africa and all that. Ndio tukasema tufanye Lava Lava . The video imefanyika tayari I am sure you have seen the pictures.

Kuhusu anavyoathiriwa na mfumo wa digitali

Yah it’s affecting a lot of wanamuziki I think, makampuni especially kwa watu ambao tunategemea TV kujitangaza kama mimi as Shaa nimeona asilimia kubwa ya my fans wangu wanasema Hawajaona video yangu ya Promise mpaka leo. In a way I feel kwamba that’s affecting me kwasababu ni a new song that I wanted to push na ndio maana nikatoa video na kuisambaza kwenye TV Station.

Kwahiyo inaniumiza kinamna ingawa siku hizi vijana wajanja zaidi my fan base ni vijana kwahiyo wapo sana kwenye Facebook kwenye blogs and website kwahiyo wameiyona. Ingawa ningependelea vile vile kwamba kuwe na urahisi wa wao vile vile kuiona kwenye TV kwenye comfort ya nyumbani kwao, kwasababu hata mama yangu I had to go and show her kwenye laptop yeye nyenyewe alikuwa haoni ITV haoni EATV. So imeniaffect kinamna halafu kubwa sana. Lakini naamini kwamba as long as your focus is not hapa nyumbani tu, haikuaffect kihivyo.

Ushauri wake kwa serikali

Kama walivyofanya muda ule wa kuregister simu walitangaza wakatupa muda kwahiyo hata mtu unajiandaa. Halafu hata huko kijijini ndio usiseme, halafu viewership, show nyingi ndio huko mikoani. Kwahiyo I don’t think we were ready na ving’amuzi nyenyewe ni utata, yaani kama unakaa eneo lenye majengo utata, I don’t think we were ready kwakweli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents