Technology

Facebook yapanga kutumia ndege zisizo na rubani na satellite kusambaza internet duniani

Theluthi ya idadi ya watu wote duniani haina access na Internet. Facebook tayari ina zaidi ya watumiaji bilioni 1, lakini kabla haijampata kila mtu duniani ni lazima kila mmoja awe na access na internet.

140327182558-facebook-drone-story-top

Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii imetangaza hatua mpya katika hamu yake ya kupeleka internet isiyo na gharama kwa kila mtu duniani.

Maabara mpya ya Facebook kuhusu upatikanaji wa internet itafanya utafiti na kujaribu teknolojia ya ndege zisizotumia rubani (drones) pamoja na satellite kusambaza huduma ya internet katika maeneo ambayo hayana kwa sasa.

“Tumekuwa tukifanyia kazi njia ya kuwapa watu internet kutoka angani,” alisema CEO wa mtandao huo, Mark Zuckerberg.

Teknolojia hiyo itahusisha ndege hizo zitakazokaa angani kwa miezi kadhaa na kuwapa watu internet katika maeneo ya mbali. Kufanikisha hilo, Facebook imechukua wataalam kutoka NASA na timu iliyotengeneza ndege ya Zephyr inayotumia jua.

Soma zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents