Technology

Facebook yawasaidia wananchi wa Zambia kupata internet bure kwenye simu zao kupitia app

Mradi wa Facebook uitwao Internet.org umechukua hatua mpya katika lengo lake la kuwapa internet watu ambao hawapo online bado, kwa kuanzisha app yake jana nchini Zambia.

Facebook

App hiyo ya Internet.org itawapa watumiaji wa mtandao wa Airtel nchini humo access ya huduma mbalimbali za internet bure. Watumiaji wa app hiyo hawatalipia tena gharama za data ambazo kwa watu hali ya chini hawawezi kuzimudu katika kupata baadhi ya huduma za internet.

Facebook imekuwa ikizungumza na makampuni ya simu duniani ili kuanzisha huduma yake ya bure ya internet kama njia ya kuwaunganisha watu wote duniani kwenye mtandao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents