Afya

Fahamu kuhusu ugonjwa wa Tetenas

Tetenasi  usababishwa na bacteria wanaoitwa ( Clostridium tetani). Bacteria hawa wanapatikana katika mazingira yanayotuzunguka mfano; ardhi, misumari au vitu vyenye ncha, vinyesi vya baadhi ya wanyama nk.


Bacteria wa tetenasi wanaweza kuishi katika mazingira kwa miaka mingi. Pia wanapenda vidonda, ndio maana wanaingia mwilini kupitia vidonda au mikwaruzo.

Dalili za ugonjwa wa Tetenasi. 

Kuna dalili kadhaa za mtu aliye na ugojwa wa tetenas ila hizi ni baadhi kati ya hizo zingine:-

  1. Kukakamaa kwa misuli, mdomo kushindwa kufunguka(lock-jaw)
  2. Kutokwa na jasho jingi, homa kali
  3. Kushindwa kumeza kwasababu ya kukakamaa kwa misuli.
  4. Kutokwa na udenda(drooling).

Jinsi ya kujitibu:

  1. Fika kituo cha afya mara baada ya kupata jeraha lolote ili kupata chanjo ya tetenasi.
  2. Kwa wafanyakazi wa afya, ni muhimu kupata chanjo ya tetenasi kwasababu ya mazingira hatarishi  ya kazi.
  3. Epuka majeraha yasiyokua ya lazima, vaa viatu, weka vitu vyenye ncha kali mbali na watoto.
  4. Mfanyie suna mtoto hospitalini na sio kwa mtaani, kwasababu ya hatari kubwa iliyopo ya kupata tetenasi.

 Chanzo:Mtandao

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents