Fainali ya ‘REDE’, mshindi anachukua ‘Vijora 20, Mbuzi wawili (+Video)

Fainali ya mchezo wa rede kupitia michuano ya Mrs Nyamwija Super Rede Cup inatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi hii, katika viwanja wa Hananasif Jijini Dar Es Salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari Mrs Nyamwija ambaye ni Mke wa Diwani wa Hananasif amesema kuwa ameamua kuinua mchezo huo katika Wilaya ya Kinondoni kwakuwa mchezo huo unaonekana kama vile umesahaulika.

”Mchezo wa rede ni mchezo ambao una muitikio mkubwa sana, hata tulivyofungua watua walijaa sana na nusu fainali ilijaza watu wengi,”

Kwa upande wa wawashindi Mrs Nyamwija amesema ”Mshindi wa kwanza ataondoka na kombe, Mbuzi wawili na Vijora 20. Mshindi wa pili ataondoka na vijora 10 na Mbuzi wawili na mshindi wa tatu ataondoka na vijora 10.”

IMEANDIKWA NA @fumo255

#Bongo5Updates

Related Articles

Back to top button