Burudani

Fainali za ‘The Jump Off Michano’ kufanyika Jumamosi hii

Fainali ya shindano la The Jump Off Michano lililoandaliwa na kituo cha redio cha Times FM zitafanyika Jumamosi hii kwenye viwanja vya Dar Live jijini Dar es Salaam.

11899540_527718694046515_1268853229_n

Shindano hilo limedumu kwa kipindi cha miezi mitatu.

“Shindano la The Jump Off Michano lilikusanya vijana zaidi ya 32O ambao wanafanya muziki wa rap pekee,” mtangazaji wa kipindi cha The Jump Off Saleh Jabir ameiambia Bongo5.

“Mpaka kufikia sasa wamebakia vijana 10 ambao watachuana wikiendi hii pale Dar Live.

“Dhumuni la shindano hili ni kusupport muziki wa rap na wanahipop kwa ujumla na kuibua vipaji vipya hii ni kwa sababu muziki wa rap na utamaduni wa hiphop ulionekana kukosa nguvu inayostahili kwa vyombo vya habari na kusababisha malalamiko ya mara kwa mara toka kwa wana hiphop wakiamini hawapati nafasi ya kutosha katika radios za hapa nyumbani,” amefafanua Saleh.

11881738_1630329137184792_1416708229_n
Jabir Saleh, mtangazaji wa kipindi cha The Jump Off cha Times FM

“Kipindi cha The Jump Off cha Times FM kimekua ni sehemu ya maendeleo ya muziki huo hapa nchini na kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo shindano hili na kuwa na chart ya rap za nyumbani pekee ingawa pia kinatoa nafasi sawa na aina zingine zote za muziki.”
“Hivyo Jumamosi hii tutatafuta mshindi ambaye atapata nafasi ya kufanya kazi na maproducer wakubwa Hermy B na Jorsbless sambamba na pesa taslim kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu.”

Jabir amesema wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Weusi, Roma, Madee, Billnass, Chemical, Msaga Sumu na Dogo Jaxime

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents