Habari

Fanya hivi kama unataka kukuza ujuzi wako katika sehemu yako ya kazi

Kwenye soko la ushindani wa ajira ni muhimu kujifunza kila siku na kukua katika taaluma yako. Kumbuka kwamba muda hautoshi na ni nadra sana kupata muda huo ili uweze kujifunza.

012312-national-black-women-values

Imekuwa ngumu sana kufanya kazi ipasavyo na uweze kupata muda wa kuendeleza taaluma yako kwa maisha ya baadaye, kama taaluma ni kitu cha msingi kabisa inatakiwa uje na mbinu zitakazo kusaidia kukuza taaluma yako na kama unataka kupandishwa cheo unahitaji kuthibitisha kwamba una uwezo huo.

Vitu vitano vitakavyokusaidia kuongeza ujuzi hapo hapo kazini ni kama ifuatavyo; inahitaji uendelee kuongezea taaluma yako ufahamu na weledi ili kuonyesha kwamba unastahili hicho unachotaka; hapa nitakuonyesha unafanyaje:

Pata mshauri na wewe uwe mshauri

Kuwa na mshauri wa taaluma yako ni jumbo muhimu sana itakusaidia kupata ujuzi mpya na hata ufahamu wako kuongezeka. Mshauri mzuri atakusaidia kupambana na changamoto na namna ya kuzitatua. Mshauri mzuri atakusaidia namna nzuri ya kuchukua hatua na kuweza kuona pale ambapo hukupaona vizuri.

Vile vile mshauri mzuri atakusaidia kujua kitu gani unachopaswa kusikia na sio kile ambacho unapenda kusikia. Unachotakiwa kupata ni mshauri wako wa taaluma au maisha yako atakupa mtizamo ambao hujawahi kufikiri au kuutazamia na kama huna mshauri wa hivyo unahitaji kutafuta kwa nguvu zote.

Uwe tayari kupokea changamoto mpya

Unapoona fursa mpya unatakiwa ujifunze na uipate. Je kuna kitu ambacho kampuni au sehemu yako ya kazi wanataka kukianzisha? Unatakiwa kujua na ufanye jitihada kujifunza ujuzi unaohitajika kwa ajili ya jumbo hilo na ulikabili. Unatakiwa kuweka jitihada ya ziada ili uweze kukua na kuongezeka katika taaluma yako. Watu wanaofanikiwa kwenye taaluma zao huwa wepesi wa kujifunza na kuchangamkia fursa, hawapendi kuwa eneo hilo hilo kila mwaka wanataka kufikia malengo fulani, wewe unataka kufikia wapi? na je umechukua hatua gani?

Usome na kutafuta matatizo ya kutatua

Ninaelewa niko kwenye jamii ya watu ambao ukizungumzia kusoma wanawaza wanafunzi na kwamba hawahitaji kusoma tena, utakuwa umekosea sana kama unafikiria kusoma ni kuongeza cheti au kupata stashahada ya juu. Hapa tunazungumzia uwezo wako wa kutatua changamoto na uwezo wako wa kuelewa mambo katika kazi hiyo unayoifanya.  Unatakiwa uwe ni mtu uliyebobea katika hicho unachokifanya kiasi kwamba mtu akifikiria kukutoa lazima ahesabu gharama ya kumpata mtu kama wewe. Ukiona wewe unaondolewa ondolewa kirahisi rahisi inamaanisha thamani yako ni ndogo sana kiasi kwamba ni rahisi kupata mbadala wako.

Tafuta marafiki wanaofanya kazi idara zingine

Mara nyingi ukitaka kupata ujuzi mpya huo unapatikana kwenye idara zingine na kwa kupata majukumu tofauti na unayopata kila siku kwenye idara yako. Ili uweze kushinda hili unahitaji kutengeneza mtandao wako wa ndani ya kampuni hiyo, nikimaanisha kuchukua jukumu la kufahamiana kwa ukaribu na undani na wale watu ambao si wa idara yako na kujua wanachokifanya kama unaweza kujifunza hapo ndipo utaweza kujifunza kama unawake ukaribu na watu wengine.

Tafuta Kujua kama kuna fursa za wewe kujifunza hapo hapo ndani ya kampuni

Hiki ni kitu cha mwisho ambacho huwa kinasahaulika. Makampuni mengi yana mfumo wa mafunzo ya ndani ili kuweza kusaidia idara mbalimbali. Hivyo unatakiwa utafute kwa juhudi yote na hata kama kuna gharama zinahitajika unatakiwa kujipanga kwa hilo. Ingawa wale ambao wanaishi kwa mgawo wa semina elekezi hawawezi kunielewa kabisa ni mpaka pale watakaoambiwa hawahitajiki na kugundua hawana ujuzi ambao wanaweza kustahili ushindani wa soko kwa sasa.

Kupata ujuzi mpya haimaanishi kwanza masomo ya jioni, mara nyingine ujuzi unaohitaji uko hapo hapo elope ni jukumu la kujua na namna ya kupata ujuzi huo.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents