Habari

For Single Ladies: Yule mwanaume aliyedaiwa kufukuzwa Saudi Arabia kwa kuwa ‘ Handsome’ kupitiliza adai yuko single na anahitaji girlfriend (Video)

Unakumbuka ile story ya mwanaume handsome aliyesemekana kufukuzwa Saudi Arabia kutokana na kuwa handsome kupitiliza? Kama hukuisoma isome hapa.

Al gala-4

Mwanaume huyo Omar Borkan Al Gala ambaye uhandsome wake umemfanya amepata umaarufu sehemu mbalimbali duniani, alifanyiwa interview na kudai kuwa hakufukuzwa Saudi kutokana na kuwa ‘too handsome’
“Really, I was walking around, I ended up in the wrong place at the wrong time” alisema Al Gala ambaye ni muigizaji, na mpiga picha kutoka Dubai.

Al gala-5

AL gala mwenye miaka 25 ameonekana kuwa kivutio cha kinadada wengi hata hapa nyumbani Tanzania, ambapo wiki hii mtangazaji wa Clouds FM Diva Loveness Love alidiriki kusema yuko tayari kubadili dini ili aolewe na huyu jamaa hata kama ana wake wengi!

“Hata dini ntabadili wallah… Anioe tu huyu kaka .. Hata mke wa ngapi poa @omarborkan isn’t he just a cute man on earth guys?” Aliandika Diva Instagram baada ya kupost picha ya Omar.

Al gala-3

Al gala-diva

Well, good news kwa Diva mwenye ndoto za kummiliki kijana huyu mtanashati ni kuwa, alitangaza kuwa yuko single na anatafuta girlfriend (na hakusema deadline ya applications-LOL).

“Yeah I’m single. I am looking for a good princess that actually could keep up with me” alisema Al Gala wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari wa Philippines.

Tazama mahojiano hayo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents