Michezo

Haji Manara awajibu wanaokosoa utendaji kazi wake

Baada ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara hapo jana Septemba 31 kufanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea adhima yao ya kufikisha nakala za barua kwa TFF, Bodi ya ligi TPLB na kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusiana na kutoridhishwa na baadhi ya maamuzi yaliyofanywa na waamuzi katika baadhi ya michezo yao iliyopita.

Hii leo Manara kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ameeleza namna baadhi ya watua anaowaita magwiji wa ukosoaji walivyo mshutumu kwa kile alichozungumza.

“Kiasili Haji Manara sio mtu dhaifu anayeweza kukalia kimya shutuma zinazokuja kwake binafsi au taasisi anayoingoza na kuifanyia kazi, ni aina ya mtu anayejua thamani ya habari, anaetaka na kuamini usahihi wa jambo liliopo na linalokuja kwa kadri lilivyo.” Amesema Haji Manara

Manara ameongeza “Nimeanza na dokezo hilo kusudi ili tuende sawa kwanza, ili kujibu tuhuma na shutuma zinazoelekezwa na baadhi ya magwiji wa ukosoaji nchini hususan kwenye tasnia yetu hii ya kandanda nchini.”

“Baada ya mkutano wangu na vyombo vya habari hapo jana jnne ya tarehe 31-10-2017 pale klabuni Msimbazi, kumetokea wakosoaji wakubwa dhidi yangu binafsi, na wengine wakienda mbali zaid kwa kunifananisha hata na msemaji wa klabu ya Yanga.”

“Nianze na hili la maudhui ya mkutano wangu wa jana na wanahabari.”

“kwanza niweke wazi kama mtu nnayesimamia idara ya Habari ya klabu, sina mamlaka yoyote ya kuitisha press bila idhini ya uongozi wa klabu ya Simba, na ktk hili simjui yoyote afanyae kazi kama yangu mwenye mamlaka ya kuongea na waandishi bila idhini ya Uongozi wa taasisi anayoifanyia kazi.”

“Kwa muktadha huo, press yangu ya jana ina baraka zote za uongozi wa Simba SC, na maudhui ya nilichokizungumza jana ni matakwa halali ya uongozi. Lakini pia niuarifu umma kuwa bado ninaamini pamoja na wanadaam kutokuwa wakamilifu, waamuzi waliochezesha mchezo wa jmosi dhidi ya Yanga na wale waliochezesha michezo mingine niliyoizungumzia jana, kuna makosa waliyafanya na mm kama msemaji wa klabu, ilikuwa ni wajibu wangu kuzungumzia hilo.”

“Inawezekana labda kwa baadhi ya watu haikuwa sahihi kwao, lakini dhamira ya klabu ya Simba sio kushutumu, bali ni kutaka ‘fair game’ hatutaki kupendelewa wala kuonewa, na ndio maana nilitoa TV Set ofisini kwangu na kuileta kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu, ili kile nnachokiongea kipate legitimacy na sio kuleta porojo za mtaani.”

“Bahati mbaya sana wale wakosoaji badala ya kujikita na hoja zangu, wakaamua kunishambulia binafsi, na hata walipoamua kujibu hoja waliegemea kishabiki zaid, huku wakiangalia dhamira za wachezaji bila kuangalia uhalisia wa kisheria na matakwa ya pigo la penati linatol.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents