Habari

Haki Elimu na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu walaani tukio la kupigwa mwanafunzi Mbeya

Shirika la Haki Elimu na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, wamelaani kitendo cha adhabu ya kikatili aliyopewa mwanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya Day, Sebastian Chinguku na walimu wa shule hiyo.

mrcun5tg

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage amesema vitendo kama hivyo vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto wengi hususani wa kike kuacha shule hivyo kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Pia ameishauri serikali juu ya uboreshaji wa utoaji wa taarifa dhidi ya matukio ya kikatili kama hayo yanapotokea.

“Serikali inapaswa kuanzisha mifumo rasmi ya kutoa taarifa dhidi ya matukio ya ukatili yanayoendelea katika shule zetu itakayowawezesha wanafunzi na wadau wengine kutoa taarifa mara wanapokutana na matukio ya kikatili kama haya kwa lengo la kuyakomesha,” amesema.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa serikali inatakiwa kuboresha miongozo yake ya kusimamia na kuimarisha nidhamu shuleni na kuhakikisha inazingatiwa na watu wote.

Kwa upande wake Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kimepongeza mshikamano uliooneshwa na wananchi katika kukemea ukatili huo.

20161007095602-page-001

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents