Burudani

Harmonize achomoa ‘kumchinjia baharini’ Willy Paul

Baada ya msanii Will Paul kutokea nchini Kenya kuachia ngoma yake ‘Pilipili’ ambayo alimshirikisha Harmonize, kuliibua tetesi nchini humo kuwa wawili hao wana bifu.

Chanzo cha taarifa za kuwepo bifu hilo ni baada ya Harmonize kutoonena ku-support wimbo huo kwa upande wa hapa Bongo baadala yake kuwa bize na kazi na zake.

Sasa katika show ya 10 over 10 ya Citizen TV, Kenya, Harmonize amesema hakuna kitu kama hicho bali kilichotokea ni kutoelewana ila urafiki wao upo pale pale.

“Mimi napenda mtu ambaye anapenda ku-push muziki wake ufike mbali ndio kitu ambacho kinafanya hata mimi napata nafasi ya kufanya kazi na wasanii wa nje,” amesema.

“Nafikiri ni kutokuelewana tu wakati tunatoa wimbo huo, kwa sababu siwezi kutumia muda nikarekodi wimbo, nika-shoot video halafu nisi-push, nitakuwa nimefanya kazi ya bure,” ameongeza Harmonize.

Ameendelea kwa kusema kuwa menejimet ya Will Paul na yake (WCB) ndio ratiba ziliingiliana lakini hakuna ugomvi kati yao. Wimbo wa Will Paul na Harmonize ‘Pilipili’ ulitoka April 07, 2018 na hadi sasa una views 762,570 katika mtandao ya You Tube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents