Habari

“Hatutapakia abiria watakaobeba mizigo yao kwenye mifuko ya plastiki”

Chama wa wamiliki wa mabasi Tanzania (TABOA) kimewataka wamiliki wote wa mabasi nchini kuanzia kesho Juni mosi kutopakia abiria wenye mizigo iliyowekwa katika mifuko ya plastiki ili kutekeleza agizo la Makamu wa Rais pamoja na sheria na kanuni za mazingira zinazoanza utekelezaji wake juni mosi mwaka huu.

Akizungumza katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo, mweka hazina wa (TABOA) amewataka madereva na makonda kutekeleza agizo hilo na kudai (TABOA) hakitakubali kumtetea mmiliki yeyote atakaye kaidi agizo la serikali kwa kuruhusu abiria wenye mizigo iliyowekwa kwenye mifuko ya plastiki.

Wakizungumza na kituo cha runinga cha ITV baada ya jiji la Dar es Salaam kuwa la kwanza kutekeleza agizo hilo, baadhi ya wananchi wameitaka zoezi la kuzuia mifuko ya plastiki kwenda sambamba na uwekaji wa vituo vya kukusanya mifuko hiyo katika mitaa ili kuiondoa katika mazingira.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents