Burudani

Hawa ni mastaa ambao Marekani inatamani wangekuwa ni raia wa nchi yao

Kuna mastaa ambao waliwahi kufanya vizuri kwenye muziki na bado wengine wanaendelea kufanya vizuri lakini nchi ya Marekani wanatamani kama wangekuwa ni miongoni mwa raia ambao wanatokea nchini kwao.

Dr.-Shein-e1440500563622

Japo nchi ya Marekani imebahatika kuwa na mastaa wengi ambao wanafanya vizuri kwenye industry ya muziki duniani, lakini kuna ladha za baadhi ya wasanii ambao imekosekana kwenye nchi hiyo kwa muda mrefu.
Hawa ni baadhi ya mastaa ambao Marekani inatamani kama wangekuwa ni wazawa wa nchi yake.

Adele

1401x788-GettyImages-162588693

Jina lake halisi ni Adele Laurie Blue Adkins, alizaliwa mwaka 1988 nhini Uingereza kwenye mji wa London.

Adele amehitimu mafunzo ya muziki kwenye chuo cha Brit School for Performin Arts and Technology, mwaka 2006. Mwaka 2007 alisaini mkataba na XL Recording na albumu yake ya kwanza iliofahamika kwa jina la ‘19’ aliyoitoa mwaka 2008.

Mpaka sasa hivi Adele ameshafanikiwa kuachia albumu tatu ‘19’ mwaka 2008, ‘21’ mwaka 2011 na ‘25’ mwaka 2015. Adele ameshafanikiwa kuwa nominated kwenye tuzo 201 na amefanikiwa kupata tuzo 102 tangu ameingia kwenye muziki mpaka sasa, zikiwemo tuzo za Grammy, Brit Award, Billboard Music Award, MTV European Award, American Music Award, European Border Breakers Award, na nyingine nyingi.

Pia Adele ameshafanikiwa kuweka rekodi kadhaa kwenye Billboard ambazo hakuna msanii mwengine aliyewahi kuweka, lakini kubwa zaidi ni wimbo wake wa ‘Hello’ ambao umefanikiwa kuangaliwa mara bilioni mbili kasoro huku ukifanyiwa Cover na wasanii.

Celine Dion

Dr.-Shein-e1440500563622

Celine Dion ni mmoja kati ya wasanii wakubwa na wenye heshima kubwa sana duniani. Mpaka sasa ana umri wa miaka 48 akiwa ni raia wa nchi ya Canada.

Celine Dion ni miongoni mwa wasanii matajiri duniani akiwa na utajiri wa dola milioni 630. Tangu ameanza kuimba akiwa na umri wa miaka 12, Celine Dion amefanikiwa kupata tuzo 300 kati ya tuzo 400 alizowahi kushiriki.

Mpaka sasa Celine Dion amefanikiwa kuachia nyimbo zisizopungua 378, kati ya hizo amefanikiwa kuimba kwa kutumia lugha za nchi tofauti kama vile; Kiingereza, Kichina, Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano, Kilatini na Kijapani.

Uwezo wake wa kuimba kwa kupanda hadi kugusa key ya mwisho ndiyo umewavutia watu wengi na kumfanya kuwa maarufu zaidi duniani. Kutokana na rekodi aliyoiweka Celine Dion na uwezo aliokuwa nao hakuna msanii kutoka nchini Marekani ambaye ameweza kuikaribia rekodi yake.

Aubrey Drake Graham

drake

Drake ndiyo jina ambalo linafahamika zaidi kwenye industry ya muziki duniani. Ni raia wa nchi ya Cannada, lakini ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, muandaaji wa muziki na muigizaji pia.

Drake ambaye yupo chini ya lebo ya Young Money Entertainment (YME) aliyosaini mwaka 2009, inayomilikiwa na Lil Wayne.

Nyimbo yake ya ‘Best I Ever Had’ ilifanikiwa kushika namba mbili kwenye list ya Billboard Hot 100 na albumu yake ya ‘Thank Me Later’ ilifanikiwa kushika namba moja kwenye Billboard 200.

Drake amefanikiwa kuchukua tuzo za Grammy, tuzo 3 za Juno Awards, tuzo sita za BET Awards. Kutokana na uwezo wake amefanikiwa kushirikishwa kwenye nyimbo kibao na wasanii wa kubwa kama Jazz, Kanye West, Rihanna, Rick Rose na wengine wengi.

Kutokana na uwezo wake kuandika nyimbo nzuri na kipaji cha kuimba Hip Hop na RnB ndiyo unawavutia watu wengi na kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii bora wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye industry ya muziki duniani.

Justin Bieber

photo

Bieber ni miongoni kati ya wasanii waliopata umaarufu wakiwa na umri mdogo. Mpaka sasa Bieber ana umri wa miaka 22 lakini ameshafanikiwa kufanya mambo mengi kwenye industry ya muziki ambayo inamfanya awemaarufu dunia nzima.

Pia Bieber amefanikiwa kupata tuzo kibao zikiwemo za Billboard Music Award, Grammy Award, MTV European Music Award na nyingine nyingi.

Bieber amefanikiwa kuachia albamu nne mpaka sasa, ‘My World 2.0’ mwaka 2009, ‘Under The Mistletoe’ mwaka 2011, ‘Believe’ mwaka 2012 na ‘Purpose’ Novemba 2015. Albumu yake ya nne ilifanikiwa kuuza kopi milioni 44.7 kwa nchi ya Marekani na iliuza kopi milioni 75 kwa dunia nzima, pia imefanikiwa kuingia kwenye list ya kuwa ni mwa albumu zilizouza kopi nyingi duniani.

Justin Bierber amefanikiwa kuingia kwenye top ten ya Forbes Magazine kwa mara tatu mfululizo kama ‘Most Powerful Celebrities’. Pia amewahi kuwa msanii wa kwanza video yake kupata views bilioni kumi kwenye Vevo.

Japo amekuwa ni msanii mwenye vituko vingi kwa kipindi cha nyuma na kupelekea kuachana na mpenzi wake, Selena Gomez ilionekana kuwa ulikuwa ni utoto lakini kwa sasa ameonekana amebadilika kuja kwa vingine akianzia kwenye wimbo wake wa ‘Sorry’ uliofanikiwa kupata views zaidi ya bilioni moja na milioni 218 na bado anaendelea kufanya vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents