Burudani

Billnass azungumzia tuhuma ya kuwa TID anatumia madawa ya kulevya

Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya Radar Entertainment, Billnass amesema kuwa hajawahi kumuona TID akitumia Madawa ya Kulevya kama maneno yanavyoongelewa mitaani.

Bill Nas

Akizungumza katika kipindi cha The Playlist cha Times Fm Jumamosi hii, rapa huyo ameshangazwa na maneno hayo ambayo amedai hajui yanatokea wapi.

“Sijui haya maneno yanatokea watu, ni vitu ambavyo watu wanatumia kwa siri sana ila mimi sijawahi kumuona TID akitumia, na tunasafiri kila kwenda sehemu kibao hata dalili za mtu anayetumia madawa ya kulevya sijawahi kuziona kwa TID. Sijui sijawahi kumuona kwa kweli”, alisema

Billnass kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao ‘Chafu Pozi’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents