Burudani

Hawa ni wasanii waliotoka ‘from zero to hero’ mwaka 2015

Mastaa wengi duniani ukiulizia historia ya maisha yao huwezi kuamini utakachosikia lakini huo ndio unabaki kuwa ukweli.

Wasanii

Mwaka 2015 ulikuwa na neema kwa baadhi ya wasanii wa Bongo ambao kwa muda mfupi wamekuwa mastaa bila hata ya wao wenyewe kutegemea. Hakuna mafanikio yanayokuja mbele pasipo kujituma, hawa wanaweza wakawa ni baadhi ya wasanii wengi waliotokea kwenye hali ya chini ndani ya Tanzania, mwaka 2015 ukawa wa bahati kwao.

Kayumba Juma

12825704_187939761579415_1814819335_n

Bongo Star Search (BSS) season 5, ndio iliyomtoa Kayumba Jr, kuwa mshindi wa shindano hilo na kufanikiwa kushinda shilingi milioni hamsini. Ukisikiliza historia ya maisha ya Kayumba hutaweza kuvumilia lazima utatokwa na machozi.

Kayumba alijituma na kuhangaika pasipo kukata tamaa mwaka 2015 ukawa wa neema kwake, amefanikiwa kumiliki gari yake na amenunua kiwanja na kuanza ujenzi kwa ajili ya nyumba ya familia yake.

Kwa sasa hakuna asiyemfahamu Kayumba, wakati mwaka mmoja nyuma hakuna aliyekuwa anamfahamu kipindi alipokuwa anatembea kwa mguu kutoka Manzese mpaka Magomeni akiwa hana nauli na njaa ikimuuma.

Harmonize

12797798_872760259499772_1419178477_n

Aiyola ni moja kati ya nyimbo nzuri zilizowahi kuwavutia watu wengi, hilo lilimfanya mpaka msanii wa Nigeria, Kiss Daniel kutamani kumtafuta Harmonize ili wafanye collabo.

Mwaka moja nyuma hakuna aliyemjua Harmonize, juhudi zake na kipaji chake cha kuimba na kuandika kilimvutia Diamond Platnumz kumuingiza kwenye lebo ya Wasafi.

Hutaweza kuamini Harmonize akikwambia alishawahi kuweka makazi kwenye kituo cha mabasi akiwa hana kwa kuishi, ukikutana naye leo hutaweza kuamini aliwahi kuuza chai pale Kariakoo, hayo yote aliyoyapitia hakuwahi kukata tamaa alijituma mpaka mafanikio yalipomfikia 2015.

Ruby

12716988_950387361735358_1219392776_n

Ruby ni zao kutoka THT, ni mmoja kati ya wasanii wenye sauti nzuri na uwezo mkubwa wa kuimba pasipo kubahatisha. Mwaka 2015 ulikuwa mzuri kwa Ruby baada ya kuachia wimbo wake ‘Na Yule’ ambao umefanya vizuri kwenye media kibao.

Shindano la Super Nyota Diva hataweza kulisahau mrembo huyu. Miaka kadhaa hakuna aliyeweza kumtambua Ruby, lakini kujituma kwake na kutoona aibu kuonyesha kipaji chake ndiko kulimfanya mwaka 2015 uwe wa neema kwake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents