Michezo

Haya ndio maamuzi ya FA kuhusu kadi nyekundu ya Feghouli

Kiungo wa klabu ya West Ham, Sofiane Feghouli baada kupewa kadi nyekundu katika mechi ya jumatatu, ya Januari 2 dhidi ya Manchester United. Chama cha soka cha England FA kimetangaza kuifuta kadi hiyo aliyopewa kiungo huyo.

Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya West Ham kukata rufaa kupinga kadi hiyo aliyopewa kiungo huyo kutoka Algeria.

Feghouli alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi Mike Dean katika dakika 15 ya mchezo baada ya kuonekana kumchezea madhambi beki Phil Jones.

Baada ya maamuzi hayo, sasa kiungo yuko huru kucheza mechi ya FA raundi ya 3 ijumaa hii dhidi ya Man City.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents