Burudani

Hemedy PHD: Ningependa wasanii tusaidie kutoa elimu ya upigaji kura kuliko kushabikia vyama

Hemedy PHD amedai hajajifunga na chama chochote cha siasa kama ilivyo kwa wasanii wengi na kwamba jambo la muhimu zaidi ambalo anaamini wangefanya ni kusaidia kueneza elimu ya upigaji kura.

20150928215718

Hemedy ameiambia Bongo5 kuwa wananchi wengi hawana elimu hiyo na hapendi kuona limefumbiwa macho.

“Wenye haki ya kupiga kura tayari ni wengi, wengi wamekua na wengi ni wageni ambao wameingia kwenye umri wa miaka 18 na kuendelea, tofauti na sisi tuliokuwepo before,” amesema.

“Nafikiri kuna haja ya watu kuelekezwa na kuelimishwa juu ya upigaji kura, kwamba ukifanya hivi unapatia, hivi unakosea.”

Hemedy amesisitiza kuwa watu wengi pia hawajasoma na wana haki ya kupiga kura. Anahofia kuwa kura nyingi zinaweza kuharibika kutokana na wananchi kukosa elimu hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents