Burudani

Mtoto wa Chris Brown sasa ni Royalty Brown rasmi

Chris Brown na mzazi mwenzie, Nia Guzman wamemaliza vita vyao kuhusiana na haki ya kila mmoja kukaa na mtoto wao pamoja na jina lake rasmi kwenye cheti cha kuzaliwa.

11939525_857097401070900_1064040128_n

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Chris na Nia wamekubaliana rasmi kumlea pamoja mtoto huyo. Chris atakaa naye kwa siku 12 katika mwezi na hakutakuwa na usimamizi.

Kuhusiana na jina la mtoto wamekubaliana kuwa ataitwa Royalty Brown bila jina la katikati.

Chris atakuwa akimlipa Nia $2,500 kwa mwezi. Pia atakuwa akimlipa dola 15,000 kwa mwezi kama ‘back support.’

Chris pia atakuwa akimsomesha Royalty, kulipia matibabu yake na bima ya afya na gharama za walezi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents