MichezoUncategorized

Hii ndio michezo atakayeikosa Ronaldo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu UEFA

Hii ndio michezo atakayeikosa Ronaldo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu UEFA

Ikiwa ndio mchezo wake wa kwanza katika michuano ya UEFA akiitumikia timu yake ya mpya Juventus,Cristiano Ronaldo atazuiwa kucheza mechi gani, na je, kunauwezekano wowote wake kuikosa mechi dhidi ya Manchester United uwanjani Old Trafford? Manchester United wamo kundi moja ya Juve pamoja na Young Boys na Valencia. United walishinda 3-0 mechi yao.

Tofauti na Ligi ya Premia ambapo marufuku ya kadi nyekundu ya moja kwa moja huwa ni kutocheza mechi tatu, adhabu ya Uefa huangazia kwa kuzingatia kisa chenyewe.

Marufuku ya kutocheza mechi moja huwa ni lazima, na hakuna haki ya kukata rufaa. Lakini kanuni za Uefa nambari 50.01 zinazosimamia michuano hiyo zinasema “iwapo kosa litakuwa kubwa sana, jopo la Uefa linaloangazia udhibiti, maadili na nidhamu lina haki ya kuongeza adhabu hiyo.”Ronaldo, 33, bila shaka ataikosa mechi itakayofuata ya Juve Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambayo itakuwa dhidi ya Young Boys mnamo 2 Oktoba.

Iwapo marufuku itaongezwa na kuwa mechi mbili, basi ataikosa mechi dhidi ya klabu yake ya zamani Manchester United mnamo 23 Oktoba uwanjani Old Trafford.Na iwapo atapewa marufuku ya mechi tatu, basi ataikosa hata mechi ya nyumbani dhidi ya United mnamo 7 Novemba.Juve wanatarajiwa kukata rufaa dhidi ya jaribio lolote la kutaka kuongeza marufuku hiyo.

Kiungo wa kati wa zamani wa Man Utd Darren Fletcher anatarajia Ronaldo atacheza mechi zote mbili.”Ilikuwa adhabu kali kwa kosa ndogo kwa Ronaldo, lakini kwa kufuata sheria kikamilifu hauruhusiwi kufanya hivyo (hilo ni kosa), kwa hivyo nafikiri marufuku ya mechi moja itasalia,” mchezaji huyo wa Stoke kwa sasa aliambia BBC.”Atajihisi ni kama aliwakosea wachezaji wenzake, lakini natarajia acheze mechi zote mbili dhidi ya Manchester United.”

Beki wa zamani wa United Rio Ferdinand aliandika kwenye Twitter kwamba hana shaka kwamba Juve watakata rufaa. Lakini mshambuliaji wa zamani wa Celtic Chris Sutton anaamini Ronaldo anaweza tu kujilaumu mwenyewe.

Teknolojia ya kutumia video kuwasaidia waamuzi, maarufu kama VAR haitumiki katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu.Ronaldo alinusurika kuonyeshwa kadi nyekundu akichezea Ureno dhidi ya Iran katika Kombe la Dunia pale VAR ilipoonyeshwa alihitaji tu kuonyeshwa kadi ya manjano.

Na meneja wa Juve Massimiliano Allegri alisema baada ya mechi ya Jumatano kwamba VAR ingelisaidia uamuzi wa refa.Kuwa na wachezaji 10 katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kosa kama hilo ni jambo la kusikitisha. Tulihatarisha sana usiku wa leo kutokana na hili, na tutamkosa sana katika mechi zifuatazo pia.

“Alikuwa na masikitiko, lakini huchukua muda kutulia. Ni lazima aukubali uamuzi huo na awe tayari kwa mechi ya Jumapili, [dhidi ya Frosinone], hata ingawa kuna mambo yanayokuacha na machungu sana.”

  • Juventus wameoneshwa kadi 26 nyekundu katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, saba zaidi ya klabu nyingine yoyote katika michuano hiyo.
  • Juve wamepokea kadi nyekundu katika mechi tatu mfululizo za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (kwa jumla kadi tatu) kwa mara ya pili katika historia ya klabu hiyo, walifanya hivyo pia Oktoba 2000 na Septemba 2001 (kadi tano kwa jumla).
  • Aidha, wameshinda mechi zao za ufunguzi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2015-16 (2-1 v Manchester City), wametoka sare mechi moja na wakashindwa mechi moja katika hizo nyingine mbili.
  • Baada ya kwenda mechi tisa nyumbani Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya bila kushindwa (Walishinda 6 Sare 3), Valencia sasa wameshindwa mechi nne kati ya tano za nyumbani katika ligi hiyo, na kufungwa magoli 10.

chanzo BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents