Burudani

Hiki ndicho alichokisema Kingwendu baada ya kukosa ubunge

Aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Kisarawe, Rashid Mwinshehe maarufu kama Kingwendu, amesema baada ya kushindwa, anajipanga upya kwa mwaka 2020.

Kingwendu.._full

Kingwendu aliyekuwa akigombea kupitia CUF, amesema licha ya kushindwa katika chaguzi huo, ameweza kujitangaza Afrika Mashariki na kuonesha uwezo wake.

“Nimejaribu na nimeweza lakini bahati haikuwa yangu,” amesema. “Katika ushindani kuna mawili, kushinda na kushindwa. Mimi kama nimeshindwa basi sio mbaya sikati tamaa. Sasa hivi pia nitakuwa mwanasiasa,” ameongeza.

“Namuomba pia mwenyezi Mungu aniweke salama ili mwaka 2020 kama nitakuwepo hai nitaingia tena kwenye kinyang’anyiro. Nimeshajua mapungufu yangu yako wapi na kwa bahati mbaya nilikuwa sijajipanga vizuri lakini nilijitaidi. Kwa sababu nilijua ni kawaida kawaida tu kwamba nitatumia hela kidogo lakini nimekuta nimetumia nyingi na nimechemsha sana mtu wa CCM na nimetengeneza rekodi nzuri sana kwa jina langu Afrika Mashariki na hapa nyumbani. Niligombea nafasi ya ubunge nikashika nafasi ya pili, hii pia ni hatua katika maisha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents