Burudani

Hip Hop ya Tanzania yatoka kapa tena kwenye nomination za MTV MAMA

Kwa mara nyingine tena tangu kurejeshwa kwa tuzo za MTV MAMA, miaka mitatu iliyopita, hakuna msanii wa hip hop kutoka Tanzania aliyetajwa kuwania mwaka huu.

14262673_178458339228913_5424735233209532416_n

Kwa miaka yote hiyo kipengele cha hip hop kimekuwa kikienda kwa wasanii wa Nigeria na Afrika Kusini. Cha kushangaza zaidi ni kwenye kipengele hicho mwaka huu kuna wasanii wapya wakiwemo Emtee wa Afrika Kusini na Ycee wa Nigeria.

Katika mwaka ambao msanii wa hip hop kutoka Tanzania alitakiwa kupata nomination ni huu. Mtu kama Joh Makini amefanya vizuri si tu Tanzania kwa maana ya kazi zake kuonekana au kuchezwa.

Don’t Bother aliyomshirikisha AKA, ilifanya vizuri kote MTV Base, Trace na kwingine huku pia wimbo ukipenya kwenye redio kadhaa za Kenya.

Joh alipaswa kuwa mwakilishi mzuri wa hip hop kutoka Afrika Mashariki mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents