Bongo5 Makala

Hizi collabo ziliwatangaza au kuwatoa hawa wasanii 15

Wasanii kushirikiana katika nyimbo zao (collabo) si jambo baya kwani ni utamaduni wa siku nyingi na ndio msingi wa muziki wenyewe ulipoanzia. Ushirikiano huu hutumika kama njia ya kubadilishana mashabiki au kuongeza. Kwa mfano msanii wa miondoko ya hip hop anapomshirikisha msanii wa RnB ni wazi atajichotea mashabiki wapya kutoka upande wa pili.

Dogo Janja, Mau Sama, Vanessa Mdee na Darassa.

Sababu nyingine ya wasanii kushirikishana ni kumkuza mwenzake zaidi. Kwa mfano Collabo ya Diamond Platnumz na Davido ni wazi ilimkuza Diamond Platnumz na kumtangaza katika level za kimataifa.

Chukua hii ya mwisho, collabo pia humtoa msanii kimuziki, kwa mfano masanii chipukizi (underground) anapofanya kazi na msanii mkubwa ambaye yupo mainstream ni wazi anaanza kujulikana na kujichotea mashabiki wake.

Sasa leo kupitia Bongo5 nakuletea orodha ya wasanii walioshirikiana na wimbo waliotoa ukawa umemtoa mmoja wapo au kumtangaza zaidi. Narudia tena, wimbo waliotoa ukawa umemtoa mmoja wapo au kumtangaza zaidi.

  1. Shetta x Belle 9

Alianza muziki kwa miondoko ya kurap ila ngoma zake mbili za mwisho kutoa inavyoonekana amekacha miondoko hiyo. Utaniunga mkono kama ulisikiliza kwa wimbo wa Shirorobo na Namjua.

Kazi aliyofanya na Belle 9 iliyofamika kwa jina la Nimechokwa na ndo ngoma ilimtambulishwa Shetta kwenye muziki wa Bongo Fleva, hivyo ilimtoa.

  1. Maua Sama x Mwana FA

Wanadada huyu mwenye sauti ya kipekee alikuwa amesharekodi wimbo wa So Crazy na mtu mwingine huko nyumbani kwao Moshi.

https://youtu.be/lFbrR5CuFOU

Alipokuja Dar es Salaam ndipo alipokutana na Mwana FA wakaifanya upya ngoma hiyo chini ya prodyuza Marco Chali, na ndo ikawa tiketi ya Maua Sama kusikika kwenye Bongo Fleva, kwa maana hiyo ilimtoa.

  1. Darassa x Ben Pol

Walitoka na wimbo uitwao Sikati Tamaa, ngoma hii ndio iliyomtambulisha Darassa kwenye muziki wa Bongo Fleva na kumpatia umashuhuri alionao kwa sasa.

Naamini katika maisha ya kimuziki ya rapa Darassa hawezi kumsahau Ben Paul na prodyuza Maneke aliyepika ngoma hiyo, hivyo ngoma hii ilimtoa.

  1. Mabeste x Jux

Wimbo waliotoa pamoja ulitambulika kama Baadae Sana, wakati huo Mabeste alikuwa chini ya usimamizi wa B’Hit Music Group.

https://youtu.be/eFKF3iPt73o

Wakati huo Jux na wenzake waliouanda kundi la Wakacha kazi zao nyingi walizifanyia B’Hit, ni wazi ngoma hii ndo ilipelekea watu wengi kumjua Mabeste, hivyo ilimtangaza zaidi.

  1. Ommy Dimpoz x Alikiba

Ni wazi bila ubishi wimbo wa Nai Nai ndio ulimtoa Ommy Dimpoz na kumtangaza kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Wimbo ulifanyika G Record kwa prodyuza KGT, nawaza ngoma hii ingekuwa vipi bila sauti ya Alikiba, ila si deni Ommy Dimpoz tayari ameshatoka.

  1. Stamina x Rich Mavoko

Ngoma ya Kabwela waliofanya wawili hawa ndio ilimtambulisha Stamina kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Stamina aliona umuhimu wa wasanii wa kuimba katika miondoko ya rap au hip hop ndio sababu kazi yake iliyofata alimshirikisha Jux.

  1. Abukiba x Nay wa Mitego

Ngoma waliyofanya kwa pamoja na kufanya vizuri ilitambulika kama Uyo Sio Demu, ingawa kwa kipindi hicho Nay wa Mitego alikuwa msanii wa kawaida tu, si kama sasa.

Muunganiko wao ndio uliwavutia wengi hadi wimbo kufanya vizuri, na hatimae leo tunae Abukiba kwenye Bongo Fleva.

  1. Young Killer x Belle 9

Alikuwa akisifika kwa uwezo aliokuwa nao wa kuandika misitari kwenzi na kuichana kitu kilichokuwa kikiwashangaza wengi kutokana na umri aliokuwa nao.

https://youtu.be/7TlR_yfkeuU

Ngoma ya Dear  Gambe aliyomshirikisha Belle 9 ndo ilimtoa na kumpa tuzo ya KTMA mwaka 2013 kama msanii bora chipukizi.

  1. Dogo Janja x Tunda Man

Watu wengi walikuwa wakishangazwa na mtindo wake wa kurap, kilikuwa ni kipaji kipya ndani ya Tip Top Connection.

Ngoma ya Anajua aliyokwepo pia na Madee ndio ilimtambulisha kwenye muziki wa Bongo Fleva, kwa sasa amebadilisha aina yake ya muziki na anaelekea kwenye kuimba.

  1. Izzo Buzness x Suma Lee

Kipindi hiki alikuwa chini ya usimamizi wa MJ Records, ngoma waliyotoa pamoja ilifahamika kama Business kama sehemu ya jina lake.

https://youtu.be/kGhYfYU8MRA

Najaribu kuwaza pindi Izzo Business anafunga safari kutoka Mbeya kuja Dar es Salaam, hivi alikuwa anajua sauti ya Suma Lee ndio itamtoa au kumtangaza zaidi, ila si deni kashatoka na sote tunamfahamu kwa sasa.

  1. Nikki Mbishi x Ben Pol

Wakati wanafanya kazi wote wawili walikuwa chini ya lebo ya M Lab na wakafanikiwa kutoa ngoma ya Play Boy ambayo ndio iliyompa Nikki Mbishi umaharifu mkubwa.

https://youtu.be/txGvLiTMD_g

Wawili hawa wameshafanya kazi kibao pamoja kama vile Beauty na Ndo yeye, lakini Play Boy inabaki pale pale kama kazi iliyomtoa Nikki Mbishi.

  1. Vanessa Mdee x Ommy Dimpoz

Ingawa Vanessa alikuwa ameshasikika kwenye baadhi ya ngoma kama vile Money ya AY, Press Play ya Dj Choka na ngoma yake Closer, bado mashabiki wengi walikuwa hawajamuelewa sana.

Ngoma ya You and Me aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz ilimpa jina kubwa kwenye muziki na watu kuanza kumtazama kwa jicho la tatu.

  1. Dayna x Marlow

Marlaw alikuwa ameshajenga jina lake kwa kiasi kikubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva, Dayna alikuwa kama msanii mchanga ambaye alikuwa bado hajasikika masikio mwa mashabiki wa muziki huu.

https://youtu.be/23dC-T-XuZc

Ngoma ya Mafungu waliyoitoa mwaka 2009 ndio ilimtambulisha Dayna kwenye muziki huu, prodyuza aliyehusika kwenye mdundo wa ngoma hii ni Marco Chali.

  1. Mwasiti x Ali Nipishe

Hawa wote ni wasanii wa THT, ili Mwasiti amekuwepo kwa muda mrefu kwenye kundi hilo na wasanii wengine kama Barnaba na Linah.

https://youtu.be/kvZMtuRZz-8

Ngoma ya Mapito ya Mwasiti ndiyo ilimpa jina Ali Nipishe na watu wengi kumfahamu, kisha baadae akatoa ngoma yake binafsi ‘My’ ambayo ilimpaisha zaidi kwenye muziki wa Bongo Fleva.

  1. Bill Nas x Nazizi & T.I.D

Wimbo ujulikanao kama Raha ndio ulimtoa Bill Nas kimuziki. Sauti ya Nazizi kutoka nchini Kenya na ya Mzee Kigogo ‘T.ID.’ ndio ilimpa kibali cha kusikika katika Bongo Fleva.

Kipindi hiki Bill Nas alikuwa akisimiwa naRada Entertainment na ndio sababu ya sauti ya T.I.D kuja kusikika tena katika wimbo ‘Ligi Ndogo’.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents