Burudani

Hizi ni nyimbo za mastaa wakubwa zilizoandikwa na Drake

Drake ni mmoja kati ya rapper wenye uwezo mkubwa duniani japo mara kadhaa baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakimkejeli kwa madai kuwa hawezi kuandika mashairi ya nyimbo zake na amekuwa akiandikiwa.

drake sad

Ubora wa Drake ulionekana mapema mwezi Mei mwaka huu alipoachia albamu yake ya ‘Views’ iliyofanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard takribani kwa wiki sita na kufanikiwa kuvunja rekodi ya 50 Cent aliyowahi kuiweka na wimbo wake, ‘Candy Shop’.

Hizi ni baadhi nyimbo ambazo Drake amewahi kuwaandikiwa mastaa wakubwa duniani na zikafanya vizuri kwa mujibu wa Billboard.

Un-thinkable (I’m Ready) – Alicia Keys

Wimbo huu unapatikana kwenye albamu ya Alicia keys ya ‘The Element of Freedom’ yenye nyimbo 14 iliyotoka Disemba 11, 2009. ‘Un-thinkable’ ni moja kati ya nyimbo za RnB zilizowahi kufanya vizuri mpaka kushika namba moja kwenye chati za Billboard.

Sifa zote za wimbo huu zinamuendea mwandishi ambaye ni Drake ndiye aliyechangia kwa asilimia kubwa kwa wimbo huu kufanya vizuri.

30 Hours, Father Stretch My Hands & Facts – Kanye West

Hizi ni nyimbo tatu zinazopatikana kwenye albamu mpya ya Kanye West ‘Life Of Pablo’ aliyoiachia Februari 14 mwaka huu. Hakika Kanye West ataendelea kumshukuru Drake kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwenye albamu hiyo kutokana na kumuandikia nyimbo tatu rapper huyo ikiwemo ‘30 Hours’, ‘Father Stretch My Hands’ na ‘Fact (Charlie Heat Version)’.

“I wanna thank my brother Drizzy for helping me on 30 Hours & Father Stretch My Hands. Drake would come by and just help, no strings. Future also came by to write. We all got new shit together that’s gonna drop soon,” aliandika Kanye West kwenye mtandao wake wa tweeter.

Mine – Beyonce

Wimbo wa ‘Mine’ ni wimbo mwingine ambao rapper Drake mashairi yake yalitumika ndani ya wimbo huo japo wengine akiwemo producer wa Noah Shebib, Jordan Ullman, Sidney Brown, Dawne Weir na Beyonce walichangia kuuandika wimbo huo uliotoka mwaka 2013.

R.I.P – Rita Ora

R.I.P ni wimbo wa staa wa muziki wa Pop kutoka Uingereza, Rita Ora uliotoka Mei 6, 2012 ambao ni wimbo mwingine Drake ameshiriki kwa asilimia kubwa kuuandika wimbo huo japo wasanii wengi akiwemo Meek Mill aliyemdiss rapper kwa kurap, “This is hip-hop, you ain’t write it, don’t record it. I don’t know how they gettin’ down ‘cross the border.”

Hata hivyo wimbo huo uliingia kwenye utata baada ya kudaiwa kuwa ni copy kutoka kwenye albamu ya Rihanna ya mwaka 2010 ‘Loud’ lakini Ora aliiambia The Sunday Times, “RIP” wasn’t written for Rihanna. But even if it was played to her, I don’t care. As soon as I heard it, I said it was mine. I was going to fight for that song.”

Fall For Your Type – Jamie Foxx

Kwa kuonyesha dunia kuwa ana kipaji kikubwa kwenye muziki, mwaka 2010 Drake alimwandikia msanii mwenzake Jamie Foxx wimbo wa ‘Fall For Your Type’ uliotoka Novemba 12, 2010 unaopatikana kwenye albamu ya nne ya msanii huyo ‘Best Night of my Life’.

Wimbo huo ulimpatia umaarufu mkubwa Foxx na kumfanya kuonekana kama mmoja kati ya wasanii bora wa Marekani huku akiendelea na kazi zake za uigizaji.

I’ve Been That Girl – Melanie Fiona

Huu ni wimbo mwingine uliowahi kuandikwa na Drake na kutoka mwaka 2012.

Kumuongelea vibaya Drake ni kama kumtukana mamba kabla ya kuvuka mto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents